Meng Hongwei Mkuu wa taasisi ya polisi wa kimataifa maarufu kwa jina la Interpol "international police" bwana Meng Hongwei amepotea akiwa kwenye safari binafsi nchini China. Kwa mujibu wa mke wake ambae alitoa taarifa ya kupotea bwana Meng kwa ofisi kuu ya Interpool nchini Ufaransa, bwana Meng alikuwa nchini China mwezi ulopita kwa safari binafsi. B
wana Meng mwenye umri wa miaka 64 anaishi kwenye mji wa Lyon uliopo kusini mwa Ufaransa ambao ndipo yalipo makao makuu ya Interpol na aliteuliwa kuwa mkuu wa taasisi hiyo mwaka 2016. Muda wake wa kuongoza taasisi hiyo unaisha mwaka 2020. Taasisi hiyo ina ofisi katika kila nchi duniani ikiwemo Tanzania na inafanya kazi zake kwa kushirikisha kila jeshi la polisi ya nchi hizo. Moja ya kazi kubwa ya taasisi hiyo ni kuwatafuta wahalifu mbalimbali duniani, wanaotafutwa na nchi wanachama kwa kuweka picha zao katika tovuti yake. Uteuzi wa bwana Meng kulihisiwa na vyombo vya kutetea hai za binadamu kwamba zilikuwa ni jitihada za serikali ya China kuwasaka na kuwatafuta raia wote ambao wanaipinga serikali ya nchi hiyo. Serikali ya Beijing imekuwa katika harakati za kushikirisha nchi za kigeni katika kuwaorodhesha raia wake ambao wengi wanatuhumiwa kwa kujishirikisha na matukio ya rushwa na ugaidi.
==============================================================================
The head of the International Criminal Police Organisation Meng Hongwei has been reported missing by his wife. Meng Hongwei travelled to China in late September, but his wife says she has not heard from him since. French police announced his disappearance today and they are leading investigations to find him. He was born in Harbin, China, in 1953, and graduated from Peking University where he studied law before entering politics in 1972.
Interpol's headquarters in Lyon, France. According to Interpol's website, Meng has nearly 40 years' of experience in criminal justice and policing, and has held several senior positions in China including vice minister of public security. He was director of China’s coast guard and appointed deputy director of China’s State Oceanic Administration.
He also served as vice minister of public security, vice chairman of national narcotics control commission and director of national Counter Terrorism Office for China. Interpol has offices in nearly every country on the planet and works towards international cooperation between different police forces. They work together to solve crimes that cross borders, sharing information and pooling resources. The Interpol website states: ‘Our role is to enable police around the world to work together to make the world a safer place. Sources: International media outlets.
===============================================================================
Updates:
Habari mbalimbali zimeripotiwa kwamba mkuu wa taasisi ya polisi wa kimataifa Interpool bwana Meng Hongwei yupo chini ya ulinzi nchini China tangu siku ametua mjini Peking kutoka nchini Ufaransa. Bwana Hongwei ambae bado kiufundi anafanya shughuli zake nchini China akiwa waziri anaeshughulikia usalama wa raia, anahojiwa na kamati ya nidhamu ya chama cha kikomunisti cha China. Haijajulikana rasmi anahiojiwa kuhusu masuala gani jambo hlo limekumbwa na giza nene na si wizara ya usalama wala ile ya mambo ya nje ambayo walikuwa tayari kujibu masuali ya waandishi. Chini ya sheria ya uangalizi na kuwekwa chini ya ulinzi, mara zote familia ya mtuhumiwa huwa inataarifiwa ndani y masaa 24 isipokuwa kama utoaji wa taarifa hiyo utaathiri uchunguzi, kwenye hili familia ya bwana Hongwei haikuwa imepewa taarifa yoyote. Pamoja na kuwa waziri wa usalama wa raia, bwana Hongwei mwezi April alipoteza nafasi ya kamati ya maamuzi ya chama cha kikomunisti cha China. Lakini hata hivyo bwana Hongwei ana mikono mingi ambyo inaweza kuwa imeelekezwa kwake khasa mikono inayohusiana na kitendo chake cha kutoa agizo liitwalo "Red Notice" Agizo hilo alilitoa mwaka 2014 la kukamatwa kwa mfanya biashara tajiri Guo Wengui ambae alikuwa anahitajiwa nchini China kujibu tuhuma mbalimbali za rushwa. Ipo orodha ya raia wa China wapatao 44 ambao wanatafutwa na serikali ya China. Chanzo: The post of China.
No comments:
Post a Comment