Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba
kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi
zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu
walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.
Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani,
hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana.
Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali
inapochanganywa na mdalasini.
Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi
mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu
yaliyomo kwenye hii dawa asili asali yenye mdalasini
Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China
(Traditional Chinese Medicine – TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India
(ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural
treatment in the East – Tibb).
Kwa mjibu wa wataalamu wa tiba asili nchini China, mdalasini huongeza joto
mwilini. Mdalasini hutengeneza joto mwilini lijulikanalo kwa kichina kama
“yang”. Yang hutibu “yin” (yin kwa kichina humaanisha baridi). Wakati asali
yenyewe kwa asili huweka sawa usawa wa joto na baridi mwilini.
Hizi ndizo kazi 24 za ASALI iliyochanganywa na mdalasini
1. Tiba ya baridi yabisi (Arthritis).
Watu wengi wanaripoti matokeo mazuri baada ya siku chache tu za kutumia
kinywaji hiki chenye mchanganyiko wa asali yenye mdasini kutwa mara 2. Ili
kutibu baridi yabisi ongeza kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na
kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya glasi 1 ya maji ya uvuguvugu
na unywe nusu glasi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu glasi nyingine
kabla ya kwenda kulala.
Utafiti huo ulifanyika katika chuo kikuu cha Copenhagen ambako wanafunzi
walipewa asali yenye mdalasini ili kutibu baridi yabisi. Baada ya wiki 1
iligundulika kuwa wanafunzi 73 kati ya 200 walikuwa hawaonyeshi dalili tena
za ugonjwa huo. Baada ya mwezi mmoja kila mmoja alikuwa amepona na kuwa na
uwezo wa kutembea na kufanya kazi.
2. Nzuri kwa ugonjwa wa moyo
Chakula sahihi, mazoezi ya viungo, na kuepuka kukaa kwenye kiti masaa mengi
ni mhimu kwa ajili ya kuwa na afya nzuri ya moyo.
Kunywa kinywaji chenye asali yenye mdalasini mara kwa mara kunaweza kusaidia
kuepuka ugonjwa wa moyo kwa kuzuia kuzibika kwa ateri.
3. Inatibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
Asali yenye mdalasini ni dawa bora sana kwa kutibu maambukizi kwenye kibofu
cha mkojo na bacteria wowote wanaoweza kushambulia kibofu cha mkojo.
Mchanganyiko huu unasafisha kibofu na kukiacha safi hivyo kukupa mazingira
ya kutokuumwa lolote katika kibofu chako cha mkojo.
4.Huua bakteria
Asali ina sifa ya kudhibiti bakteria. Nadharia hii inathibitishwa na
tafiti nyingi kadhaa. Asali hupigana dhidi ya maambukizi ya ndani nay a
nje. Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe pia huondoa sumu
mwilini. Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili vinatengeneza
muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.
5. Huongeza akili
Watu wengi wanaripoti kuwa asali yenye mdalasini inawaongezea uwezo wao
wa kukumbuka vitu. Asali yenye mdalasini hongeza uwezo wa ubungo kufanya
kazi na kuongeza uwezo wa kumbukumbu.
6. Inatibu meno yanayotoboka
Hii kidogo inashangaza. Watafiti katika jiji la New York nchini Marekani
wanasema asali inaweza kusababisha meno kutoboka. Hata hivyo wanasayansi
wengine nchini New Zealand wanasema asali inaweza kuwa msaada katika kuzuia
meno kutoboka kutokana na sifa yake ya kuua bacteria mbalimbali.
Namna rahisi ni kutumia mchanganyika wa asali yenye mdalasini kama dawa yako
ya meno utumie kusafisha meno yako ili kuepuka meno kutoboka na kuoza pia.
7. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Husafisha utumbo mpana kwa kuondoa sumu na taka nyingine. Husaidia
uzalishwaji wa bacteria wazuri kwenye utumbo mpana na kama matokeo yake
huusadia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
8. Huondoa gesi tumboni
Asali yenye mdalasini husaidia kulinda tumbo kwa kufunika kuta za tumbo. Kwa
kusafisha mfumo wa bakteria wabaya huwa imesaidia kutibu maambukizi yoyote
na hivyo kusaidia kutibu tatizo la tumbo kujaa gesi na asidi.
9. Husaidia kupunguza uzito
Kuna shuhuda nyingi zisizotiliwa shaka juu ya ufanisi wa asali yenye
mdalasini katika kupunguza uzito. Asali na mdalasini vinapotumika pamoja,
mchanganyiko huo huchoma mafuta kwa haraka sana.
Wakati huo huo mchanganyiko huu hushusha njaa na hivyo kumfanya mtu
kujisikia ameshiba muda mrefu.
Angalizo hata hivyo, asali ni tamu na ina nguvu (kalori), hivyo ili
kupunguza uzito unashauriwa usitumie zaidi ya vijiko vikubwa vitatu vya
mchanganyiko huu ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu kwa siku,
Ukizidisha tu unaweza kuongezeka uzito tena.
10. Hutibu Fizi kutoa damu
Watafiti nchini New Zealand wamegundua kuwa asali mbichi ikichanganywa na
mdalasini inaleta ufanisi mkubwa dhidi ya fizi kutokwa damu, kuuma fizi,
ganzi kwenye meno na maambukizi mengine katika fizi.
Unaweza kupakaa kwenye mswaki na utumie kama dawa yako ya kusafisha meno ili
kupata faida hii.
11. Hutibu kansa
Ingawa bado haijathibitishwa kisayansi ni jinsi gani asali yenye mdalasini
inatibu kansa lakini uwezo wake wa kuondoa sumu na vimelea vingine vya
magonjwa (free radicals) kunaifanya kuwa na sifa hiyo ya kutibu kansa.
Baadhi ya watu wameripoti kupona kansa ya titi na kansa ya utumbo mpanakwa
kutumia asali yenye mdalasini.
12. Inaongeza nguvu ya mwili
Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una
kalsium, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).
Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga
ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza
kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.
13. Hutibu chunusi
Kupakaa asali yenye mdalasini kwenye ngozi yako yenye chunusi kutaondoa
chunusi hizo bila kuchelewa. Asali hudhibiti bacteria na mdalasini hudhibiti
maambukizi na huondoa sumu.
Mchanganganyiko huu husaidia asali kubaki juu ya ngozi kwa muda mrefu na
hivyo kufanya uponyaji unaohitajika.
14. Hutibu kikohozi
Kuinywa asali yenye mdalasini ndani ya glasi ya maji ya uvuguvugu hupunguzu
vyote kikohozi na kikohozi kikavu. Husafisha msongamano kohoni na kutibu
kikohozi cha kawaida na hata kile kikavu.
15. Huzuia madhara ya kung’atwa na wadudu
Ni nzuri kwa ajili ya uvimbe au kuondoa maumivu yatokanayo na kuumwa na
wadudu. Chukua kijiko kidogo kimoja cha asali na uchanganye ndani ya vijiko
vijigo viwili vya maji ongeza na mdalasini ya unga nusu kijiko cha chain a
upake juu ya sehemu ulipong’atwa na mdudu.
Maumivu hayo yataondoka mara moja.
16. Husaidia kuotesha nywele
Changanya kijiko kidogo kimoja cha asali ndani ujazo sawa wa mafuta ya
zeituni na uongeza kijiko kidogo cha chai tena cha mdalasini ya unga kwenye
huo mchanganyiko.
Pakaa mchanganyiko huo kichwani sehemu ambako nywele zimeanza kupotea na
uache kwa dakika 15 kisha jisafishe na maji ya uvuguvugu na shampoo ya
asili.
17. Hutibu lehemu (Cholesterol)
Matumizi ya mara kwa mara ya asali yenye mdalasini husaidia kupunguza
lehemu. Pia husaidia kushusha shinikizo la juu la damu na kusafisha ateri
zinazoziba.
Pia kubadili matumizi ya mafuta mengine na kuamua kutumia mafuta ya zeituni
kutarahisisha kuweka sawa kolesto yako kirahisi zaidi.
18. Hutibu maumivu ya jino
Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko
vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma
mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yatakapopotea.
19. Harufu mbaya mdomoni
Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali na kiasi kingine sawa cha
mdalasini ya unga ndani ya maji glasi moja ya uvuguvugu na unywe mara tu
ukiamka asubuhi. Hii itakutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni na utapumua
vizuri bila shida yoyote.
20. Hutibu uanithi na kukosa hamu ya tendo la ndoa
Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye
mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo
kwa dakika 15 hivi.
Kunywa nusu glasi asubuhi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu nyingine
kabla ya kwenda kulala kwa siku kadhaa hata wiki kadhaa.
21. Huongeza kinga ya mwili
Ongeza kinga yako ya mwili na magonjwa hayatakugusa. Vyote asali na
mdalasini hupigana dhidi ya bakteria na virusi na hivyo kufanya dawa nzuri
ya kupigana na kuua bakteria wabaya na virusi.
Asali pia ina madini na vitamini mhimu nyingi hivyo kuupa mwili viinilishe
mhimu unaovihitaji.
22. Hutibu mafua
Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali yenye mdalasini ndani
ya glasi moja ya maji ya uvuguvgugu kutwa mara moja kila siku kuondoa chafya
na kuvimba koo.
23. Hutibu Ugumba
Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote
wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya kwenda
kulala kila siku.
Mdalasini umetumika miaka mingi katika dawa za kichina na kihindi kuongeza
uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.
24. Faida nyingine lukuki
Kumbuka asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa na watu wamekuwa wakiitumia
kutibu magonjwa mengine mengi bila idadi ikiwemo matatizo ya kisukari,
kukakamaa kwa miguu na mikono, udhaifu wa jumla wa mwili, kuongeza
kumbukumbu, vidonda vya tumbo, kutibu majeraha nk.
Hizi ndizo kazi 24 za asali yenye mdalasini ambazo ulikuwa huzijui bado.