MAAMBUKIZI kwenye njia ya mkojo ( Urinary Tract Infection kifupi U.T.I) ni maambukizi yanayoshika nafasi ya pili kuupata mwili mara nyingi zaidi.
Maambukizi haya hufanya mtu kukosa raha na kwa baadhi ya watu hasa wanawake ni tatizo la kiafya linalojirudiarudia mara nyingi.
Kwa bahati mbaya ni kwamba tiba iliyozoeleka kwa U.T.I ni kutumia dawa za kuua bakteria (antibiotics) ambapo bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanaoitwa E.coli wameanza kuwa sugu dhidi ya hizi dawa hivyo kusababisha wagonjwa wengie kupata U.T.I sugu.
U.T.I ni mkusanyiko wa maambukizi eidha ya fangasi, virusi au bakteria ambayo yanatokewa kwenye njia ya mkojo ya mwanamke na mwanaume. Tunaposema njia ya mkojo tunaongelea figo zote mbili, mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo huitwa ureter, kibofu chenyewe na mrija wa kutoa mkojo nje kutoka kwenye kibofu.
Kazi ya figo ni kuchuja maji yaliyopo kwenye damu na kutoa maji yaliyozidi na takamwili. Baada ya hapo mkojo huifadhiwa kwenye kibofu na baadaye kutolewa nje kupitia mrija wa urethra ambayo una misuli ya sphincter iliyopo kwenye uke na uume.
Bakteria wanaopatikana kwenye kinyesi ndiyo kwa kiasi kikubwa husababisha U.T.I. Hawa wanapoingia kwenye njia ya mkojo mwilini kwa kutumia kinga yake huweza kuwadhibiti, lakini inaposhindikana ndipo bakteria hawa husababisha madhara.
Kitendo cha kukojoa mara kwa mara husaidia kusafisha bakteria waliojishikiza kwenye njia ya mkojo na pia tezi dume hutoa majimaji kwa mwanaume ambayo huzuia ukuaji wa bakteria wabaya. Japo kuna kinga kubwa ya mwili dhidi ya U.T.I lakini bado kuna hatari ya kuugua ugonjwa huu ndiyo maana tunatakiwa kuwa makini zaidi.
KWA WANAWAKE
Wanawake wapo hatarini zaidi kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo kutokana na kwamba njia yao ya mkojokuelekea kwenye kibofu ni fupi kwa hiyo bakteria wanaweza kusafiri haraka zaidi na kuleta athari kwenye kibofu. Sababu nyingine ni kwamba njia ya kutolea mkojo kwa mwanamke kwenye uke ipo karibu zaidi na mahali pa haja kubwa penye bakteria waletao maambukizi.
DALILI ZA U.T.I
Zifuatazo ni dalili za moja kwa moja kwa watu wazima kupatwa na ugonjwa huu kama vile kupata maumivu makali wakati wa kukojoa, kujisikia hali ya kuchomachoma kwenye kibofu wakati wa kukojoa, kujisikia kukojoa mara kwa mara na kutoa mkojo mdogo sana, maumivu ya misuli, maumivu chini ya tumbo, mkojo kuwa mwekundu au wa pink (dalili ya damu kwenye mkojo) na unaonuka na maumivu ya nyonga kwa wanawake na wakati mwingine kushindwa kujizuia mkojo.
AINA ZA MAAMBUKIZI
Kuna aina nyingi za maambukizi katika njia ya mkojo.
Maambukizi yanayotokea kwenye mirija ya urethra huitwa Urethritis na dalili zake ni kama maumivu ya mgongo wa chini, homa kali, mwili kutetemeka na kutapika, urethritis yaweza kusababishwa na bakteria wa E. coli na virusi pia wa herpes simplex. Kama maambukizi yametokea kwenye kibofu basi huitwa cystitis.
Dalili za athari kwenye kibofu ni kama maumivu ya nyonga, mkojo wa mara kwa mara unaoambatana na maumivu makali na mkojo wenye damu.
Bakteria pia wanaweza kusafiri mpaka kwenye figo na kuathiri figo, aina hii ya maambukizi tunaita pyelonephritis. Dalili za kuwa figo zimepata athari ni maumivu wakati wa kukojoa hii ni kutokana na uwepo wa mawe ya figo ambayo hukwama kwenye mirija ya kutolea mkojo. Maambukizi kwenye njia ya mkojo hutokea pale bakteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo, kujishikiza na kuanza kukua mpaka kuleta athari.
KWA TIBA YA UTI SUGU NA UNAPONA KABISA ANGALIA KWENYE VIDEO HII
Usisahau kusubscribe, kulike na kushare