Popular Posts

Monday, 21 January 2019

PROPHET BUSHIRI SAVED FROM HOT SOUP...WHY DO SOUTH AFRICA WANT MAJOR 1, TO STAY

Few days ago.

Review this

 JOHANNESBURG – Community members in Pretoria are calling for controversial self-proclaimed Prophet Shepherd Bushiri to pack up and go.

On Friday, a group of angry people blocked the entrance to his Enlightened Christian Gathering Church.

Stopping congregants from attending the regular Friday service.

This comes after the church was charged with defeating the ends of justice and interfering with police work for moving the bodies of three women who died during a stampede in the church last week.

The police also accused the congregation of moving the bodies of the victims to a private mortuary without reporting the incident to the police.

“We cannot have a situation whereby this Nigerian prophet doesn’t make money in his own country and decide to come here [South Africa]. If they are prophets, they must go back to Nigeria and make money there. Enough is enough; we cannot lose our loved ones, people who die like their animals. He can’t even apologise to South Africans,” South African National Civic Organisation Tshwane treasurer Abram Mashishi.

But now why South African want prophet Bushiri to stay?

Answer

Their lives have changed since they connected with the great servant of God

Alot of them they were blind,  no vision because demon closed them but after coming of Major 1, prophet Bushiri they were disconnected from devil spirit


So how about you? What do you think about this?

Sunday, 20 January 2019

IJUE HOMA YA MAPAFU ILIYOPELEKEA VIFO VINGI 2018 NCHINI TANZANIA


Homa ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani.

Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu.

 Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ambapo nembo ya siku hiyo ni nguo za rangi ya bluu.

 Muundo wa Mapafu Mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa (bronchi) ambayo hugawanyika kufanya mirija midogo zaidi ya hewa (bronchioles), ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo ya hewa (alveoli). Vifuko hivi vidogo vya hewa (alveoli) vina mishipa ya kupitisha damu (capillaries) ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu na hewa chafu ya ukaa (kaboni dioksidi) kuondolewa kwenye damu na kuingizwa kwenye mapafu tayari kwa kutolewa nje ya mwili.

Kwa kawaida vifuko hivi vidogo hujaa hewa muda wote tayari kwa kusafirishwa. Inapotokea mtu akapata homa ya mapafu, vifuko hivi hujaa maji au usaha hivyo kuathiri upitishaji wa hewa safi kwenye damu na kusababisha tatizo la kupumua.

 Homa ya mapafu husababishwa na nini?

Kuna aina kadhaa ya vimelea ambao vinaweza kusababisha maambukizi ya mapafu. Vimelea hivi hujumuisha bakteria, virusi, parasite na fangasi.

Vimelea hawa hushambulia mwili wa binadamu kulingana na umri na kinga ya mwili. Kwa mfano, bakteria wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wachanga ni tofauti na wale wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wakubwa.

Baadhi ya vimelea wa bakteria wanaoshambulia watoto ni pamoja na Streptococcus pneumoniae ambao ni aina ya bakteria wanaoongoza kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.

Wapo pia Haemophilus influenzae aina b (Hib) ambao ni aina ya pili ya bacteria walio maarufu zaidi kwa kusababisha ugonjwa wa homa mapafu kwa watoto. Staphylococcus aureus ni aina nyingine ya bacteria ambao hushambulia zaidi watoto wachanga.

Kuna pia Group B streptococci ambao pia hushambulia zaidi watoto wachanga. Kwa upande wa virusi, virusi wa aina ya Respiratory syncytial virus ndiyo wanaoongoza kwa kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.

Aidha, vimelea wa Pneumocystis jiroveci ambao kwa sasa huwekwa kwenye kundi la parasite ni maarufu zaidi miongoni mwa parasite wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wenye upungufu wa kinga mwilini hususani watoto wenye VVU.

Aina nyingine za bakteria ambao hushambulia zaidi watoto wakubwa ni pamoja na Mycoplasma pneumonia naChlamydia pneumonia. Jinsi Homa ya Mapafu inavyoenezwa Kuna namna nyingi za kuenea kwa homa ya mapafu. Kwa kawaida, virusi na bacteria hupatikana katika sehemu ya juu ya mfumo wa njia ya upumuaji (upper respiratory tract).

 Inapotokea kinga ya mwili ya mtoto imeshuka kwa sababu yeyote ile, vimelea hivi huweza kusambaa na kufika mpaka sehemu ya chini ya mfumo wa njia ya upumuaji (lower respiratory tract) na hatimaye kushambulia mapafu. Hali kadhalika, vimelea hawa wanaweza kuenea kwa njia ya damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya kuzaliwa yaani kipindi cha mimba.

 Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu

Dalili za vichomi au homa ya mapafu kwa watoto hutegemea na umri wa mtoto. Kwa watoto wadogo,

dalili za awali zinaweza kuwa:

 homa kali pamoja na mtoto kuhangaika na kunyong'onyea.

Watoto wanaozaliwa wakiwa na uambukizi wa bacteria aina ya Streptococcus kundi B wanaweza kuwa na homa na kupumua kwa shida.

Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na dalili ambazo si maalum (no-specific symptoms) kama vile kuhangaika na kushindwa kunyonya au kula vizuri bila kuwa na dalili yeyote ya kushindwa kupumua.

 Hali hii inaweza kutokea kwa mtoto wa umri wowote ule.

Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:

homa Kuhisi baridi ,kikohozi Kupumua kwa haraka kuliko kawaida kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua, Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua, maumivu ya tumbo, kupoteza hamu ya kucheza, kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya, Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto.

 Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu.

 Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.

 Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.

Vihatarishi vya homa ya mapafu (risk factors)

Katika hali ya kawaida kinga ya mtoto mwenye afya njema humlinda asishambuliwe na vimelea vinavyosababisha magonjwa mbalimbali. Hali huwa ni tofauti pale ambapo kinga ya mtoto ni ndogo au dhaifu, kwa vile mfumo mzima wa ulinzi huathirika na hivyo basi inakuwa ni rahisi kwa mtoto kupata homa ya mapafu.

Mfumo wa kinga wa mtoto unaweza kuwa dhaifu kwa ukosefu wa lishe bora hasa kwa watoto wachanga ambao hawanyonyeshwi ipasavyo.

 Aidha uwepo wa magonjwa mengine, kwa mfano, maambukizi ya VVU, saratani na ugonjwa wa Surua hupelekea kinga ya mwili kuwa dhaifu.

Lakini vile vile kuna mazingira yanayoweza kusababisha mtoto kuwa katika hatari ya kupata homa ya mapafu mfano moshi wa sigara, au moshi ndani ya nyumba unaosababishwa na kupikia kuni au mkaa.

 Vilevile msongamano ndani ya nyumba kutokana na watu kuwa wengi sehemu moja nayo huweza kusababisha watoto kupata homa ya mapafu.

 Uchunguzi na Vipimo Daktari humchunguza mtoto mgonjwa kwa kusikiliza dalili za ugonjwa kutoka kwa mzazi/mlezi wa mtoto, kuchunguza viashiria vya ugonjwa huu na kisha kumpima mtoto kwa kutumia kifaa kinachosaidia kusikia sauti mbalimbali katika mfumo wa hewa wa mgonjwa kiitwacho stethoscope.

Ili kujiridhisha na kuwa na uhakika wa tatizo hili, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kulingana na mazingira na upatikanaji wake. Vipimo hivyo ni pamoja na X-ray ya kifua, au CT-scan ya kifua, pamoja na damu ili kuchunguza madhara yaliyoletwa na homa hii ya mapafu. Faida ya kipimo cha CT-scan ni ule uwezo wake wa kutofautisha aina tofauti za homa ya mapafu na aina ijulikanayo kama Atypical pneumonia ambayo si rahisi kuonekana kwa kutumia X-ray ya kawaida ya kifua. X-ray ya kifua na CT-scan ya kifua kwa pamoja vina uwezo wa kuonesha tatizo hata pale ambapo daktari ameshindwa kusikia sauti maalum kwa kutumia kifaa chake cha stethoscope.

 Matibabu

Maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara nyingi antibiotics ndizo hutumika katika kutibu homa ya mapafu inayosababishwa na maambukizi ya bakteria. Kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi, antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu.

Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

 Namna ya kuzuia Homa ya mapafu 

Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na ya kutosha na mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi. Kuzuia homa ya mapafu kwa watoto ni sehemu muhimu ya mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya watoto. Chanjo dhidi ya Hib, pneumococcus, surua na kifaduro ni njia mojawapo ya kuzuia homa ya mapafu.

Lishe ya kutosha ni muhimu kwa kuboresha kinga ya mwili ya mtoto ambapo inashauriwa mama kunyonyesha mtoto bila kuchanganya na kitu chochote walau kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.

Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara ni jambo linaloshauriwa pia. Hii inasaidia kupunguza idadi ya watoto kupata homa ya mapafu. Kwa watoto wenye VVU, matumizi ya dawa ya cotrimoxazole kila siku husaidia kupunguza uwezekano wa kupata homa ya mapafu.

 Utafiti umeonyesha kwamba kinga na tiba sahihi ya homa ya mapafu inaweza kuzuia vifo milioni moja kwa watoto duniani kila mwaka. Hivyo ni wajibu wetu sote kushirikiana kupambana na ugonjwa huu wa homa ya mapafu

Saturday, 19 January 2019

DAWA YA KUTIBU MAGONJWA YA NGOZI KWA SIKU 7 TU.




Dawa hii inaitwa Kibiriti Upele au Sulphur kwa kizungu ambayo inapatikana kwenye maduka ya dawa asilia kwa gharama isiyozidi 5000|= tu, 

KAZI

Inatibu kabisa magonjwa yote ya Ngozi kama Chunusi, Tetekuwanga, upele,mba, miwasho mbalimbali na mengine mengi. 

NAMNA YA KUANDAA

Unachotakiwa kufanya ni kuchanganya dawa hii na mafuta ya kupaka mfano Vijiko viwili vya chakula viwekwe kwenye mikopo cha 250 mls cha mafuta ya mgando na changanya vizuri kabisa 

MATUMIZI

 Utajipaka kutwa mara tatu kwa siku 7, kwa uwezo wa Mungu ugonjwa unaokusumbua utakuwa umepona kabisa. 

Usisahau kushare kulike na kucomment

Thursday, 10 January 2019

HOW TO MAKE FREE LOGO ONLINE FOR SELL



To make your own Logo just follow 3 steps:



 1.Fill in your Brand Fill in your Brand and select your desired logo category. We have logos designs for every sector

 2.Choose your Free Logo Design Browse trough more than 10.000 logo designs that you can fully customize. Select the one that you like!

 3.Edit & Download your Logo With our Logo Creator your can customize, icons, fonts, colours, text and more. Make your Logo and download


 If you need your best logo design click link below👇👇👇
www.tailorbrands.com
Just for free 

Tuesday, 18 December 2018

IJUE U.T.I NA MATIBABU YAKE


MAAMBUKIZI kwenye njia ya mkojo ( Urinary Tract Infection kifupi U.T.I) ni maambukizi yanayoshika nafasi ya pili kuupata mwili mara nyingi zaidi.

Maambukizi haya hufanya mtu kukosa raha na kwa baadhi ya watu hasa wanawake ni tatizo la kiafya linalojirudiarudia mara nyingi.

Kwa bahati mbaya ni kwamba tiba iliyozoeleka kwa U.T.I ni kutumia dawa za kuua bakteria (antibiotics) ambapo bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanaoitwa E.coli wameanza kuwa sugu dhidi ya hizi dawa hivyo kusababisha wagonjwa wengie kupata U.T.I sugu.

U.T.I ni mkusanyiko wa maambukizi eidha ya fangasi, virusi au bakteria ambayo yanatokewa kwenye njia ya mkojo ya mwanamke na mwanaume. Tunaposema njia ya mkojo tunaongelea figo zote mbili, mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo huitwa ureter, kibofu chenyewe  na mrija wa kutoa mkojo nje kutoka kwenye kibofu.

Kazi ya figo ni kuchuja maji yaliyopo kwenye damu na kutoa maji yaliyozidi na takamwili. Baada ya hapo mkojo huifadhiwa kwenye kibofu na baadaye kutolewa nje kupitia mrija wa urethra ambayo una misuli ya sphincter iliyopo kwenye uke na uume.

Bakteria wanaopatikana kwenye kinyesi ndiyo kwa kiasi kikubwa husababisha U.T.I. Hawa wanapoingia kwenye njia ya mkojo mwilini kwa kutumia kinga yake huweza kuwadhibiti, lakini inaposhindikana ndipo bakteria hawa husababisha madhara.

Kitendo cha kukojoa mara kwa mara husaidia kusafisha bakteria waliojishikiza kwenye njia ya mkojo na pia tezi dume hutoa majimaji kwa mwanaume ambayo huzuia ukuaji wa bakteria wabaya. Japo kuna kinga kubwa ya mwili dhidi ya U.T.I lakini bado kuna hatari ya kuugua ugonjwa huu ndiyo maana tunatakiwa kuwa makini zaidi.

KWA WANAWAKE
Wanawake wapo hatarini zaidi kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo kutokana na kwamba njia yao ya mkojokuelekea kwenye kibofu ni fupi kwa hiyo bakteria wanaweza kusafiri haraka zaidi na kuleta athari kwenye kibofu. Sababu nyingine ni kwamba njia ya kutolea mkojo kwa mwanamke kwenye uke ipo karibu zaidi na mahali pa haja kubwa penye bakteria waletao maambukizi.

DALILI ZA U.T.I
Zifuatazo ni dalili za moja kwa moja kwa watu wazima kupatwa na ugonjwa huu kama vile kupata maumivu makali wakati wa kukojoa, kujisikia hali ya kuchomachoma kwenye kibofu wakati wa kukojoa, kujisikia kukojoa mara kwa mara na kutoa mkojo mdogo sana, maumivu ya misuli, maumivu chini ya tumbo, mkojo kuwa mwekundu au wa pink (dalili ya damu kwenye mkojo) na unaonuka na maumivu ya nyonga kwa wanawake na wakati mwingine kushindwa kujizuia mkojo.

AINA ZA MAAMBUKIZI
Kuna aina nyingi za maambukizi katika njia ya mkojo.

Maambukizi yanayotokea kwenye mirija ya urethra huitwa Urethritis na dalili zake ni kama maumivu ya mgongo wa chini, homa kali, mwili kutetemeka na kutapika, urethritis yaweza kusababishwa na bakteria wa E. coli na virusi pia wa herpes simplex. Kama maambukizi yametokea kwenye kibofu basi huitwa cystitis.

 Dalili za athari kwenye kibofu ni kama maumivu ya nyonga, mkojo wa mara kwa mara unaoambatana na maumivu makali na mkojo wenye damu.

Bakteria pia wanaweza kusafiri mpaka kwenye figo na kuathiri figo, aina hii ya maambukizi tunaita pyelonephritis. Dalili za kuwa figo zimepata athari ni maumivu wakati wa kukojoa hii ni kutokana na uwepo wa mawe ya figo ambayo hukwama kwenye mirija ya kutolea mkojo. Maambukizi kwenye njia ya mkojo hutokea pale bakteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo, kujishikiza na kuanza kukua mpaka kuleta athari.

KWA TIBA YA UTI SUGU NA UNAPONA KABISA ANGALIA KWENYE VIDEO HII


Usisahau kusubscribe, kulike na kushare

Sunday, 16 December 2018

NJIA KUMI (10) ZA KUONDOA CHUNUSI NA MABAKA MABAKA MWILINI


1. Magadi Soda,
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge hicho sehemu iliyoathirika na chunusi.
Kwa muda wa dakika 15 hadi 20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa majiyasiyo ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapoona athari za chunusi zimepotea.


2. Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
Matango ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha likae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 hivi, kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu hadi utakapopona.

3. Kitunguu Swaumu:
Unaweza kutumia kitunguu swaumu kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu swaumu huleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bakteria sababu kina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili ya kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili).
Twanga kitungu swaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi huku ukishikilia kwa dakika 5 mpaka 10, na kisha safisha na majibaridi. Waweza kufanya hivyo asubuhi na jioni

4. Mnanaa (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni. Majani ya mnanaa hutumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa.
Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

5. Limao:
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.

6. Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

7. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

8. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.
Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

9. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.

10. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe namazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.
Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

Wednesday, 12 December 2018

KIJANA WA MIAKA 14, ALIYEHUKUMIWA KUNYONGWA



KIJANA MDOGO WA MIAKA 14 ALIYEHUKUMIWA KUNYONGWA

 GEORGE JUNIUS STINNEY, Jr.  ndiye kijana mdogo aliyehukumiwa kifo kwa kiti cha umeme mwaka 1944, baada ya wasichana wawili wa kizungu, Betty June binnicker wa miaka 11 na Mery Emma thames wa miaka 7.    baada kupotea na miili yao kuokotwa kesho yake ikiwa tayari wamekufa na mtu wa mwisho kuonekana akiongea na hawa watoto alikuw ni huyu kijana mwenye asili ya kiafrika George(14)

ANGALIA TUKIO ZIMA KATIKA VIDEO HII

                 R.I.P George  stinney, jr (14)

HOT CRL COMMISSION REPORT TO ECG CHURCH RELEASED

Prophet Shepherd bushiri confirmed that ... The CRL Commission has just released the findings of their Section 7 Investigation into w...